Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Sunday, October 28, 2012

willow smith amuandikia 2pac barua........

Willow Smith ameonesha picha ya barua yake aliyomuandikia legend wa music wa Hip Hop duniani, Tupac Shakur aliyefariki hata kabla ya Willow kuzaliwa
Huku hili likitokea, bado ule uvumi kwamba mama yake na Willow Smith, Jada Pinket Smith alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Late Tupac Shakur na kwamba inawezekana waliamua kutengeneza (danganya) mazingira ya kifo chake na yeye kuhamia Cuba.
Imekuwa ngumu kuuzima uvumi huo kwani posthumous albam saba zake Tupac zimeshaachiliwa baada ya kifo chake na sasa vitu hivyo vinaonekana kumuathiri pia mwanamziki huyu mchanga mwenye miaka 11 kutokana na post yake ya hivi karibuni ikionesha barua hiyo inayosomeka!!


Dear Tupac,
I know you are alive someplace. I think that my mommy misses you. Can you come back so mommy and me can be happy! I wish you were here … I really do!
Love, Willow

Jada Pinkett amewahi kuuongelea uhusiano wake na Shakur adharani kwama 2010 katika Kipindi cha Televisheni cha WJLB Morning Show.

Alisema kuwa yeye na Pac hawakuwahi kuingia katika mapenzi ila wote wawili ila anaamini wote wawili walikuwa na hisia hizo. ni zaidi ya mapenzi ya kawaida yaliyokuwepo kati yangu mimi na yeye yaliyotufanya tuishi pamoja kama dada, wakati mwingine mama, mtoto,  baba, au uhusiano wa kirafiki. Tulikuwa tunatambua kwamba kama tungeamua kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi tusingedumu kwani wote kwa kipindi hicho tulikuwa moto. Tungeunguza kila kitu! Hivyo tukaona ili kuendelea kudumisha uhusiano uliokuwepo hakukuwa na njia nyingine zaidi kwani tungeweza kuuana sisi kwa sisi!

Kutolewa kwa barua hii kumekuja ikiwa ni muda mfupi tuu tangu kuwepo uvumi pia kwamba Jada Pinkett-Smith amepewa talaka na Will Smith hivyo hawapo tena pamoja na habari hizo zilitolewa na Essence magazine.

0 comments:

Post a Comment