Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Wednesday, December 26, 2012

PAH ONE WAJA NA MIPANGO NA STAILI MPYA

Wasanii wa kizazi kipya hapa nchini maarufu kama Pah one baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki wao kuhusiana na kazi zao za muziki,sasa leo wameamua kufunguka na kusema kwamba mwakani kila mmoja ataanza rasmi kuandaa album mpya na sababu iliyowafanya mpaka kufanya hivi ni mashabiki  kwa mujibu wa Nahreel anasema kwamba wameamua mwakani kila mmoja atakuwa akifanya ngoma au album lakini  kuhusu  Pah one itabaki kuwa pale pale na sio kama ndiyo imekufa ila watapumzika kwa muda mfupi kwa ajili ya kila mmoja akiandaa single mpya kwa mashabiki zao.Info kamili by Nahreel.

WEUSI ON THE STAGE AT MAISHA CLUB

Wasanii wa muziki wa Hip Hop kutoka A Town city maarufu kama Weusi,baada ya kufanya vizuri katika ngoma zao na mpaka kupeleka mashabiki kukubali kazi zao,sasa jana katika club ya maisha walikuwa wakitoa burudani kali zaidi huku walisindikizwa na Enika pamoja na Ben Pol.
                                                                      Nikki wa Pili
                                                                          Mashabiki
                                                            Nikki wa Pili na Lord Eyez
                                                                Mzee wa maktaba Bonta

                                                                G Nako na Lord Eyez
                                                                Joh Makini na G Nako


                                                                Millard Ayo na Marafiki
                                                                        Ben Pol
                                                                   Dunga na Enika
                                                                        Weusi!!!!!!!!    

Thursday, November 29, 2012

serengeti boys yaerekea kufuzu kombe la mataifa ya afrika


Farid wa Serengeti Boys akichuana na Ondongo
TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kuichapa Congo Brazaville bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana mwakani.
Alikuwa ni mchezaji chipukizi Mudathiri Yahya aliyeifungia Serengeti Boys bao pekee katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza kwa mpira wa adhabu uliompita kipa wa Congo Brazaville, Ombandea Mpea katikati ya miguu ‘tobo’ na kujaa wavuni.
Kwa matokeo hayo sasa Serengeti Boys watalazimika kufanya kazi ya ziada kulinda ushindi wao huo watakapokuwa jijini Brazaville wiki mbili zijazo kwenye mchezo wa marudiano ili kukata tiketi ya kwenda Morocco.
Kocha Jacob Michelsen alisema mchezo ulikuwa mgumu kwa vijana wake, lakini anawashukuru kwa kupata ushindi huo.
“Nimefurahi tumeshinda ingawa ni ushindi mwembamba, sasa tunahitaji kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mechi ya marudiano,” alisema Michelsen.
Serengeti Boys sasa inahitaji ushindi au sare yoyote ili iweze kurudia rekodi yake ya mwaka 2003 walipokata tiketi ya kwenda Gambia, lakini waliondolewa kushiriki kwenye michuano hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kubainika walitumia wachezaji waliozidi umri akiwamo Nurdin Bakari wa Yanga.
Katika mchezo wa jana, Congo walionekana kucheza kwa kujiamini na kutumia pasi fupifupi, lakini ngome ya Serengeti ilikuwa makini kujilinda na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Katika dakika ya 14 mchezaji Seleman Bofu wa Serengeti Boys aliangushwa nje kidogo ya eneo la 18 na beki wa Congo hivyo mwamuzi Miiro Nsubuga kutoka Uganda alitoa adhabu iliyopigwa na Mudathiri na kwenda moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe kwa mashabiki wachache waliojitokeza uwanjani hapo.
Baada ya bao hilo, Congo waliamka na katika dakika ya 26 bado kidogo wangepata bao la kusawazisha baada ya mpira wa kona wa Ibara Vinny kuunganishwa kwa kichwa na Obassi Gambo na kupaa juu kidogo ya lango la Serengeti.
Katika dakika ya 32, mchezaji Hussein Ibrahim wa Serengeti Boys aliwatoka mabeki wa Congo na kupiga shuti lililodakwa na kipa Mpea.
Vijana wa Congo walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo, lakini washambuliaji wake walikosa mbinu za kuipenya ngome ya Serengeti Boys ambao wenyewe walikuwa wakicheza kwa kujihami na kutumia mipira mirefu na kushambulia kwa kushtukiza.
Kipindi cha pili vijana wa kocha Michelsen walirudi uwanjani kwa kasi zaidi na katika dakika ya 59 shuti la Mudathiri la umbali wa mita 35 lilitoka sentimita chache.


777 rihanna tour 2012.


Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake
“Are you ready for Mexico? Are you ready for tequiiiiiiila? Sit down, buckle your seat belts, and let’s get drunk,” ni sauti ya Rihanna inayosikika kwenye ndege ya Boeing inayomzungusha kwenye ziara yake aliyoipa jina la 777. 777 maana yake ni siku 7 za tour katika majini 7 ya nchi 7 duniani.
Wakati ndege ikiwa angani mashabiki wa Rihanna waliopata bahati ya kualikwa kwenye tour hiyo pamoja na waandishi wa habari wapatao 150 kinachooendelea ni kula bata na mtungi kwa kwenda mbele.
Katika wakati mmoja safari hiyo iliingia dosari kidogo baada ya mwandishi mmoja kuamua kuvua nguo zake wakati ndege ikiwa hewani na kuamsha kelele na shangwe nyingi kwenye ndege hiyo.
Safari hiyo imeingiwa na dosari baada ya Rihanna kukataa kufanya interview na mwandishi yeyote na kumfanya mtangazaji huyo wa Fox FM ya mjini Melbourne, Australia kuvua nguo zake.
Wengine wanalalamika kuwa Rihanna amekuwa akitumia muda mwingi amejifungia kwenye chumba cha dharura.Pia huduma ya chakuka kwenye ndege hiyo imekuwa ikilalamikiwa na watu hao wanaodai kulishwa vyakula vya ajabu ajabu.
Wengine wanadai kuwa hawana muda wa kupumzika licha kufikia kwenye hoteli za kifahari ambako hulala kwa saa mbili au tatu tu kabla ya kuamshwa tena kuanza safari ya nchi nyingine.
Leo Rihanna atakuwa na show jijini London na tayari ameshaperfom Mexico City, Toronto, Stockhom, Berlin na Paris.
Hizi ni baadhi ya picha za ndani ya ndege hiyo na zile anazotumbuiza kwenye ziara hiyo.


Wednesday, November 28, 2012

"unapologetic" yashika nafasi ya kwanza kwenye billboard chart

 


Rihanna amefanikiwa kuiingiza moja kwa moja albam yake mpya Unapologetic kwenye chart za albam 200 za Billboard.
“Unapologetic,” iliyokamata nafasi ya kwanza pia kwenye iTunes katika nchi 43 ikiwa masaa tu tangu itoke November19, iliuza kopi 238,000 kwa mujibu wa Billboard.
Wimbo wa kwanza kutoka kwenye albam hiyo, “Diamonds” upo kwenye top five ya Billboard Hot 100 wiki iliyopita na kuwa single ya 12 ya Rihanna kuwahi kukamata nafasi ya kwanza.
Albam hiyo imefanyiwa promotion ya uhakika na Rihanna aliyefanya ziara ya siku saba kwenye majiji saba duniani kote kwa kusafiri na waandishi wa habari pamoja na mashabiki wake.


baadhi ya picha za mazishi ya sharo millionea



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.