Msanii
Naseeb Abdul ama wengi tunavyomjua kama 'Diamond' BAADA ya kutamba kwa
muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, amesema anafikiria
kujitosa katika muziki wa Mipasho / Mduara, Taarabu au vyovyote vile utakavyopenda kuuita.
Diamond amenukuliwa akiyasema hayo Jijini Dar es Salaam wiki hii
kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa kwake na muziki huo wa
taarab. Mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema
anajua uamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wake wengi, lakini ni
jambo la kawaida kwa msanii.
Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa
kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa
nchini. Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki
kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo ambayo imempatia
umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho, Diamond anasema hakuna
kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki. Ameongeza pia yeye
bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya
tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio
kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva na kwamba anaweza kufanya kila
aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba nyimbo aina zote, hivyo
endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki wa taarabu. Diamond
alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya umemfanya ajulikane sehemu nyingi
duniani, ikiwa ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali kimaisha kwa
kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki magari ya kifahari.
Sema wewe kama wewe unadhani ndo Uamuzi huo wa Diamond utamfanya aendelee kuwa Diamond huyu huyu tunayemjua?? ???
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment