Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Sunday, September 29, 2013

RAY C AVUTA JAGUAR....

STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’ameuanika ‘mkoko’(gari) wake ambao anatembelea kwa sasa aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajili hazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… Jaguar don't care...CHL means Chalamila Family.
Fungua na uutazame mkoko mpya...

MASOGANGE ATANGAZA NDOA......


MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton...Akizungumza hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.

LULU KUELEZEA MENGI KWENYE MKASI...

Wiki Iliyopita New Season ya Mkasi Ilimkaribisha msanii wa Filamu Lulu Michael kwenye kipindi cha mkasi. Hii ni baada ya kutoka Jela alipotolewa kwa dhamana. Kaa tayari kwa vipindi vya Mkasi Vinavyofata kujua Lulu aliongelea nini? Je Safari hii atatudanganya MIAKA????