Willow
Smith ameonesha picha ya barua yake aliyomuandikia legend wa music wa
Hip Hop duniani, Tupac Shakur aliyefariki hata kabla ya Willow kuzaliwa
Huku hili likitokea, bado ule uvumi kwamba mama yake na Willow Smith,
Jada Pinket Smith alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Late Tupac Shakur
na kwamba inawezekana waliamua kutengeneza (danganya) mazingira ya kifo
chake na yeye kuhamia Cuba.
Imekuwa ngumu kuuzima uvumi huo kwani posthumous albam saba zake Tupac
zimeshaachiliwa baada ya kifo chake na sasa vitu hivyo vinaonekana
kumuathiri pia mwanamziki huyu mchanga mwenye miaka 11 kutokana na post
yake ya hivi karibuni ikionesha barua hiyo inayosomeka!!
Dear Tupac,
I know you are alive someplace. I think that my mommy misses you. Can
you come back so mommy and me can be happy! I wish you were here … I
really do!
Love, Willow
Jada Pinkett amewahi kuuongelea uhusiano wake na Shakur adharani
kwama 2010 katika Kipindi cha Televisheni cha WJLB Morning Show.
Alisema
kuwa yeye na Pac hawakuwahi kuingia katika mapenzi ila wote wawili ila
anaamini wote wawili walikuwa na hisia hizo. ni zaidi ya mapenzi ya
kawaida yaliyokuwepo kati yangu mimi na yeye yaliyotufanya tuishi pamoja
kama dada, wakati mwingine mama, mtoto, baba, au uhusiano wa kirafiki.
Tulikuwa tunatambua kwamba kama tungeamua kujiingiza kwenye mahusiano
ya kimapenzi tusingedumu kwani wote kwa kipindi hicho tulikuwa moto.
Tungeunguza kila kitu! Hivyo tukaona ili kuendelea kudumisha uhusiano
uliokuwepo hakukuwa na njia nyingine zaidi kwani tungeweza kuuana sisi
kwa sisi!
Kutolewa kwa barua hii kumekuja ikiwa ni muda mfupi tuu tangu kuwepo
uvumi pia kwamba Jada Pinkett-Smith amepewa talaka na Will Smith hivyo
hawapo tena pamoja na habari hizo zilitolewa na Essence magazine.