Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Thursday, February 27, 2014

WOLPER AKANUSHA KUPIGA PICHAZA UTUPU NA MANAIKI



Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu za kibongo Jacqkline Wolper na Manaiki Sanga, anayejulikana kama The Don, wako katika bifu kubwa kisa kikiwa ni picha walizopiga pamoja.
Tukio hilo limechukua sura mpya kwenye mitandao ya kijamii baada ya wiki mbili zilizopita gazeti hili kuanika picha za mastaa kadhaa waliowahi kupiga picha zilizozua minong’ono mitaani, kutokana na tabia ya Manaiki kuaminika kuwa ni wanawake aliotembea nao...



 


Maskani Bongo liliandika juu ya Wema Sepetu kunasa kwenye mtandao wa ngono, huku likionesha picha yake kubwa akiwa na Manaiki Sanga wakiwa wamekumbatiana huku picha ndogo ndogo za wasanii wengine maarufu akiwemo Jackline Wolper nao zikiwaonyesha wakiwa na mcheza filamu huyo.

Baada ya habari hiyo kutoka, baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo walichukua kurasa za gazeti hilo na kuiweka mtandaoni na watu walipoanza kutoa maoni yao, Jack alimzungumzia Manaiki na kukanusha kuwahi kushiriki naye mapenzi.

Mjadala mkali ulizuka huku mashabiki wa wasanii hao wakisemana vikali ambapo Wolper aliomba kuelezea jinsi ilivyokuwa hadi akakutana na Manaiki, akasema “Duh yaani mimi nimekuwa mpenzi wa Manaiki tena? Huyu mshikaji alishaahidi kuwa kwa gharama yoyote atakuwa staa, hivyo akatoa mkwanja wake watu tukaula basi,” alisema Wolper.

0 comments:

Post a Comment