Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Thursday, April 4, 2013

RAY ASALIMU AMRI JUU YA FILAMU YAKE INAYO SHUTUMIWA KUUDHALILISHA UKATOLIKI ...


Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.

0 comments:

Post a Comment