Pages

Search This Blog

Powered by Blogger.

Saturday, January 19, 2013

Suarez akiri hujiangusha makusudi?????

Luis Suarez
Msambulizi wa liverpool, Luis Suarez, ana amini kuwa analengwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza lakini amekiri alijiangusha katika mechi moja ya ligi kuu msimu huu.
Katika mahojiana na kituo kimoja cha habari cha ametika ya kusini, mshambulizi huyo kutoka Uruguay, amesema kila mara yeye huangaziwa pakubwa na mashirika hayo kwa kuwa jina lake linafanya magazeti kuuza zaidi.
Suarez ambaye ndiye mfungaji bora wa liverpool msimu huu huku akiwa amefunga magoli 15, mawili nyuma ya nyota wa manchester United Robin van Persie, amekiri alijiangusha wakati wa mechi yao na Stoke City tarehe saba October mwaka uliopita.
Tangazo hilo la suarez limemuudhi kocha wa liverpool brendan roggers, ambaye amesema, mchezaji huyo ataadhibiw kuambatana na sheria za klabu hiyo.
Roggers, ametaja tangazo hilo la Suarez, kama moja ambalo kamwe halikubaliki.

Suarez amwaga mtama

Suarez sasa amewagadhabisha makocha wa timu zingine zinazoshiriki katika ligi kuu ya Premier, na pia mashabiki ambao wanahisi kuwa mchezaji huyo hujiangusha bila sababu.
Kocha wa Liverpool Brendan Roggers
Mwaka uliopita, mlinda lango wa Swansea, Ashley Williams, alisemas kuwa Suarez hujiangusha kuliko wachezaji wote ambao amewahi kucheza nao.
Mapema mwezi huu Suarez, alishutumiwa sana kuhusiana na jinsi alivyofunga bao la pili la Liverpool, baada ya kuunawa wazi mpira wakati wa mechi hiyo ya kuwania kombe la FA dhidi ya Mansfeild Town.
Lakini kocha wa Liverpoo, alimtetea mchezaji huyo akisema kwamba aliunawa mpira bila kukusudia, lakini siku iliyofuatia, vyombo vya hjabari vya Uingereza vilichapisha habari yenye mada, Suarez ni mdanganyifu na mlaghai mkubwa.
Tangu alipojiunga na Liverpool mwaka wa 2011, mchezaji huyo ameandamwa na sakata nyingi.
Amepigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi nane, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na baada ya kumaliza adhabu hiyo, alikataa kumsalimia Evra katika mechi iliyofuatia, hatua iliyomkasrisha sana kocha wa Man United Sir Alex Ferguson.

0 comments:

Post a Comment